Ushindani wa Team Kiba na Mondi unazidi kunoga hasa baada ya Mange kuwa team Kiba, na ukizingatia kiwanda cha umbea wa Tanzania kipo Instagram na Mange Kimambi ndio mzalishaji mkuu wa umbea.
Ushabiki wa Mange Kimambi kwa Kiba unamfanya awe mpinzani mkubwa wa Diamond kwa mambo mengi japo si yote.
Sasa Mondi alitoa ngoma mbili zikifuatana ya ‘One I love’ ya slow unamwambia mtoto taratibu akaongezea na Inama ft Fally Ipupa mjini mzima ukachachawa akawa ana piga vijembe kwa trending yake Youtube kuwa hakuna aliyeishusha namba moja, Akakasirika
Usiku wa kuamkia juzi akadondosha chuma kingine cha amshaamsha kinaitwa Kanyaga. Sasa mji mzima ni kelele za wana WCB hali ambayo imempelekea Mange ku-post kipande cha video akicheza huku akim-diss AliKiba kuwa amepoa kinoma mpaka mashabiki zake wanakodishwa kushangilia timu ya jirani.
Akaenda mbali na kumsema kuwa AliKiba aachane na ulezi afanye mziki, hii ni baada ya miezi kadhaa kuweka wazi kuwa mkewe Mkenya Amina amejifungua mtoto wa kiume. Na akakazia amrudishe mkeo kwao maana toka aoe hafanyi mziki. Cheki Mage alichoandika hapa chini;
@officialalikiba ona unavyotutenda fans wako, hatuna nyimbo zako za kujidai nazo mpaka tunacheza nyimbo za huyu jamaa. Haki unatuvua nguo fans wako. Embu ona fans wako tunavyotia aibuππ. Haki Embu achana na kulea bwana tuliza akili toa nyimbo za maana, unajua Dai anajikuta sana siku hizi mpaka jina lako la mfalme atakunyang’anya maana kwasasa humkuti hata robo. . . Haki mjue hapo nilikuwa nacheza huku nalia kindani ndani. Nacheza huku naumia roho nacheza nyimbo ya Dai. Ila sasa nifanyeje na huku Kiba siku hizi nyimbo zake hazieleweki ππππ. Bora hata zamani alivyokuwa anakakaa kimya mda mrefu alafu akiibuka anaibuka na dude. Hizi nyimbo zake anazotoa siku hizi zinamshushia status kishenzi. . . Yes, I said it. Ila I said it with love. Bwana tumechoka January to December tunamsikiliza Dai na wanae tuuuu, angalau kidogo Nandy analeta competition. Tumechoka bwana, @officialalikiba embu achana na ulezi bwana, kama vipi huyo mke mrudishe kwao maana toka aje hutoi mziki wa maana.( Hapo na wivu unachangia kidogo kutaka mtoto wa watu arudishwe kwao π€£π€£ππ)
Komenti za wadau sasa ndio zilipoua kabisa;
AliKiba kapoa muda mredu kidogo toka alipotoa wimbo wa ‘Mbio’ miezi kadhaa sasa na ule wa ‘Rockstar’ wakifanya pamoja na Ommy Dimpoz na Cheed. Hivi karibuni AliKiba ametambulisha lebo yake ya muziki iitawayo Kings Music ambayo wanaundwa na mdogo’ake AbduKiba, Cheed, Killy na K2ga na wimbo wao unaotesa ni wa ‘Rhumba’
DaddyCham: aliandika hivi πππamna namna chibu ni kama choo usipoenda kuoga bas utaenda kun….hata usipokunya utaenda kutupa hata mavi ya mtoto
Naye JAyfashion17 aliandika: Mondi yuko juu zaidi ya kiba tukubali,na uwepo wa mondi ndio mng’ao wa kiba.Hili picha ni kama lile la Kanumba na Ray, wanafki walikuwa wanamlinganisha kanumba na Ray,leo hi kanumba hayupo tumejionea
Neyshas alisema ππππππ₯π₯π₯πππ umeongea ukweli mm siku izi naona aibu kujiita team kiba,kabakiza sura ya kufanana na Mwanangu tu
Hamimu Kiba naye alitoa povu lake kwa herufi kubwa,…..ALIYE KUAMBIA ALIKIBA ANASHINDINA KIMZIK NI NAN? WAO NDO WANASHINDANA NA NYIMBO ZAKE,,,NA NIKUIBIE SIRI TU HAKUNA MSANII BORA DUNIAN ZAID YA ALIKIBA WALAH ALIKIBA ANAJUA NA NDOMANA HATA AKIKAAA MWAKA MZIMA BILA KUTOA NYIMBO LAKN BADO ANA HIT DADEK
No comments:
Post a Comment