Monday, June 24, 2019

Pierre Liquid na Wabunge Watua Bongo Kinyonge Baada ya kipigo cha Taifa Stars dhidi ya Senegal



Shabiki wa Taifa Stars, Pierre Liquid ni mmoja kati ya waliomo kwenye msafara wa wabunge waliorejea nchini leo kutoka Misri walikokwenda kuipa nguvu timu hiyo katika fainali za AFCON2019.

Baadhi ya wabunge waliokwenda kuishangilia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) walipozungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wakiongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wamezungumzia hali halisi ya mchezo wa jana wa ufunguzi sanjari na kutoa maoni yao juu ya ufunguzi wa mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Senegal uliomalizika kwa Tanzania kufungwa bao 2-0 na michuano ya AFCON2019 kwa jumla.

No comments:

Post a Comment