Monday, June 24, 2019

Bibi wa miaka 81 aweka rekodi kwa kuendesha Baiskeli umbali wa KM 1,545



Bibi mzee mwenye umri wa miaka 81 amekuwa mtu wa kwanza wa umri kama huo kuendesha baiskeli kutoka pembe moja ya Uingereza hadi nyingine, ukiwa ni umbali wa kilomita 1,545.

Mavis Paterson ambaye anaishi Scotland alichukua muda wa siku 23 kukamilisha safari hiyo ambayo inakisiwa kuwa ngumu zaidi. Kitabu cha rekodi ya dunia cha Guinness kimethibitisha kuwa ajuza huyo amefaulu kuwa mtu mwenye umri wa juu zaidi kukamilisha safari hiyo.

Paterson alifanya safari hiyo kama kumbukumbu kwa watoto wake wanne waliofariki miaka ya arobaini wote katika muda ya miaka minne. Ajuza huyo amefaulu kukusanya dola 64,000 itakayotumika kwenye taasisi ya ugonjwa wa saratani, Macmillan Cancer Support.

No comments:

Post a Comment