Thursday, June 27, 2019
Masharti ya Dogo Janja kwa wanaotaka kolabo
Msanii wa Bongo fleva nchini Dogo Janja ametaja vigezo viwili vya msanii kupata kolabo na yeye, kwanza lazima msanii huyo awe na kipaji cha hali ya juu au itokee neema ya Mungu ndiyo ashirikiane nayeye.
Dogo Janja ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, ambapo ameeleza kuwa si kazi rahisi kwa wasanii wa Kitazania kupata kolabo na yeye.
Dogo Janja amesema kuwa "kupata kolabo na mimi kwanza ni lazima uwe na kipaji na pili ni kudra za Mwenyezi Mungu, kwa sababu mtaani wakali wako wengi, kuliko walioko 'main stream', kwa hiyo kuna muda licha ya kipaji kudra za mwenyezi Mungu zinahitajika zaidi."
Kwa sasa Msanii huyo ameachia Kolabo aliyoshirikishwa na msanii mwenzake kutoka Lebo ya 'Manzese Music Baby' , Maarifa ambayo inaitwa 'Acha iwe'.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment