Wednesday, June 26, 2019

BREAKING: Mbunge Jaguar Akamatwa na Polisi Nchini Kenya



Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles 'Jaguar' Njagua, amekamtwa nje ya majengo ya Bunge kufuatia kauli zake za ‘kibaguzi' akiwataka wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wanaoendesha shughuli zao katika masoko mjini Nairobi na miji mingineyo kuondoka nchini humo ndani ya saa 24.

Kwa mujibu wa mtandao wa kituo cha Televisheni cha K24, Mbunge huyo amekamata leo, Jumatano baada ya kauli yake hiyo kuzua taharuki katika baadhi ya miji katika nchi zilizotajwa huku Serikali yake ya Kenya ikimkana na kusema hayo ni maoni yake na Tanzania ikiwataka Watanzania kuwa na utulivu wakati jambo hilo likishughulikiwa.

Kupitia msemaji wake, Kanali mstaafu Cyrus Oguna , Serikali ya Kenya imelaani vikali matamshi ya Jaguar na kuapa kuwalinda wafanyibiashara halali wa kigeni walioko nchi humo pamoja na mali zao.

No comments:

Post a Comment