Thursday, June 27, 2019

Nguo ya Ndani za Kim Kardashian Zawakera Wajapan



Kim Kardashian West amewaudhi watu wa Japan kwa kuanzisha mtindo wake wa vazi la kimomo unaobana maumbile ya mwili, aliouita Kimono Intimates.

Nyota huyo wa kipindi cha maisha halisi nchini Marekani amesema kuwa nembo ya nguo hiyo itakayozinduliwa Jumanne ni ya kipekee kwa ajili ya " kusherehekea na kuonyesha umbo la mwanamke ".

Wataalamu wa Japan wanasema kuwa nguo yake ya Kimomo ya ndani haifanani na kimomo cha kitamaduni cha Japan kimono
Lakini wajapan kwneye mitandao ya kijamii wamesema kuwa nembo hiyo ni ya kukosea heshima vazi lao la kitamaduni.

Kimono, ambayo ni nguo iliyouachilia mwili ambayo kwa kawaida hufungwa na mkanda mkubwa ni vazi lilianza kuvaliwa nchini Japan katika karne ya 15.

Vazi hilo ambalo linachukuliwa kama vazi la kitaifa la Japan, kwa sasa huvaliwa katika matukio maalumu.

"Tunavaa vimomo tukiadhimisha afya, ukuaji wa watoto, harusi, mahafari, katika mazishi. Ni nguo ya sherehe na hurithishwa kwa familia kupitia vizazi ," mmoja wa wanawake wa Japan Yuka Ohishi, aliiambia BBC.

"[Hizi] nguo za kubana maumbile hata hazifanani na kimomo -aliamua tu kuchagua neno ambalo lina Kim ndani yake - hakuna heshima kwa maana ya utamaduni wetu ya vazi ."

No comments:

Post a Comment