Thursday, June 27, 2019
Makonda Atua Misri Kushuhudia Mechi ya Stars na Kenya
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Stars na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasili jijini Cairo asubuhi hii tayari kwa kuongeza hamasa kuelekea mchezo wa kesho wa Taifa Stars dhidi ya Kenya.
Makonda amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Mohamed Nassoro pamoja na Rais wa TFF, Wallece Karia.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo, Makonda alisema bado anaamini Stars inaweza kufanya vizuri katika mechi zake mbili zilizosalia.
Makonda alisema kwa sasa mara baada ya kuwasili anataka kwanza kuonana na wachezaji kujua hali zao kabla ta mechi ya kesho.
Kiongozi huyo alisema shabiki kweli na mzalendo hawezi kukata tamaa baada ya Stars kupoteza mechi ya kwanza.
Alisema Stars ina wachezaji bora ambao bado wana nafasi ya kufanya vyema mbele ya Kenya iliyopoteza mechi ya kwanza pia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment