Saturday, June 22, 2019

TID amtaja adui yake na upasuaji atakaofanya



Msani it wa Bongofleva TID, ameweka wazi kuwa kitendo cha msanii Q-Chief kufurahia kupigwa kwake, kinaonesha kuwa yeye ndiye adui yake namba moja.


Akiongea kwenye Exclusive na Friday Night Live, TID amesema ''Q-Chief yeye ndio adui yangu namba moja, hapendi kuona mimi nafanikiwa ndio maana anafurahia mimi kupigwa''.

TID ambaye alipigwa siku ya Alhamis kwenye ugomvi uliotokea kati yake na watu wanaodaiwa kuwa alikuwa nao kwenye sehemu ya starehe ambapo anasema yeye ndio alisababisha ugomvi kwa kumwambia mgomvi wake kuwa anajipendekeza.

Pia ameongeza, ''Nimeshatoa ripoti polisi lakini jamaa ni wazoefu wa hizi mambo kwahiyo wamefanya tena ila mimi nitakomaa na sheria mpaka nipate haki yangu''.

Kuhusu kuumia pua yake mkali huyo wa kuimba na kucheza na jukwaa, amesema atafanya upasuaji. ''Huwezi amini pua yangu inaonekana kama Michael Jackson, ila nitaenda kufanya 'Plastic surgery' kurekebisha pua yangu''.

No comments:

Post a Comment