Wednesday, June 19, 2019
Mapenzi Sio Vita, Kwanini Tukomoane Kwenye 6X6?
Pamoja na uwepo wa manjonjo mengi katika ulimwengu wa mapenzi, kizazi hiki kisichotabirika kimeanza kugeuza tendo kuwa kama uwanja wa vita badala ya starehe inayoweza kumhamisha mtu kifikra mpaka katika ulimwengu wa kusadikika.
Vijana wengi wamekua busy kutafuta dawa za kuwafanya wawe na nguvu kupitiliza kanakwamba wanaenda vitani. Wengine wanatamba kwamba akikukamata ni mpaka kivimbe ndo akuachie. Kwani lengo ni kuumizana?
Mchezo ule hauhitaji hasira ila upole, utaratibu maalum na hisia kali zitakazo kuhamisha katika ulimwengu uliopo. Inashangaza kuona mtu ana-pump kama anazibua chemba iloziba mwaka mzima na kumsababishia kero na maumivu makali mwenza wake.
Ukifanikiwa kukaa jirani na eneo ambalo zoezi hilo huendelea unaweza kusikia kelele nyingi utadhani mtu anapigwa mangumi ila ukiuliza utaambiwa ni wapenzi wanagegedana.
Hebu tujaribu kufanya romantic love na sio vita na utaona matokeo yake, upendo utazidi kuliko awali.
Jungu kuu halikosi ukoko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment