Saturday, June 22, 2019

Kings Music Watambulisha Staili Yao ya Uno Kisilani



Wakali wanaounda Kundi la Kings Music wamefungukia kiki katika muziki sambamba na kutambulisha staili yao ya uno iitwayo uno kisirani.

Wakizungumza katika Kipindi cha Mwendokasi Drive kinachorukahewani kupitia redio hiyo, wakali hao walisema kuwa tangu wameanzisha kundi hilo hakuna kiki yoyotewaliyotengeneza na wanasonga mbele.

“Hatupendi kufanya kiki kwani siyo muziki. Sisi tumewaleteamashabiki muziki mzuri na siyo kiki. Hatupendi kiki na muzikiwetu ndiyo kiki tosha,” alisema Abdu Kiba mmoja wa wanaoundakundi hilo.

Kings Music pia walisema kwenye video yao mpya ya Rhumba dairekta ndiyo aliyependekeza kuonesha uno ambalo wao kama Kings wameshalitambulisha kama uno kisirani.

“Baada ya video kutoka tuliangalia kwa pamoja na kila mmoja akasema limependezea baada ya mmoja wetu kucheza uno hilona kuanzia hapo tukaliita uno kisirani.”

Kings Music inaundwa na wakali wengi akiwemo Abdu Kiba,Cheed, Killy na K2ga.

No comments:

Post a Comment