Saturday, June 22, 2019

Baada ya RIHANNA Kutangaza Kumburuza Mahakamani BABA yake Mzazi, Hatimaye MZEE wake Amjibu




Baada ya msanii wa muziki nchini  Fenty amesema alianza kutumia jina la Fenty kwenye  biashara zake kabla hata ya kumzaa Rihanna, Hivyo madai ya mtoto wake kuwa anamuharibia biashara yake ni ya kupuuzwa.

“Ni miaka mingi nimekuwa nikitumia jina la Fenty kwenye biashara zangu hata kabla ya yeye *Rihanna* kuzaliwa. Madai yake kuwa najinufaisha na jina la ukoo la Fenty nimeyashangaa. Nafikiri kwa kuwa jina lake limekuwa kubwa duniani hivyo anafikiri yeye ndiye wa kwanza kutumia jina hilo, ukweli ni kwamba hapana nimeanza kutumia jina hilo kibiashara muda mrefu sana.“amesema  Baba yake Rihanna, Ronald Fenty juzi Juni 19, 2019 baada ya kutoka mahakamani kuomba shtaka hilo lifutwe.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeeleza kuwa Mzee Fenty anatarajia kufungua kampuni ya Fenty Entertainment, Jambo ambalo Rihanna anahofia kuwa kampuni hiyo itakuwa haraka endapo atatumia jina la Fenty.

Kwasasa Rihanna anatumia jina la Fenty kwenye bidhaa zake za vipodozi, Ambazo ni moja ya vitu vinavyomuingizia mkwanja mrefu zaidi ukitoa muziki.

No comments:

Post a Comment