Tuesday, June 4, 2019
Baada ya kupokea kipigo, Anthony Joshua ashauriwa kumtimua kocha wake, Rob McCracken ‘Huwezi kuwa na mwali daraja la tatu’
Bondia wazamani wa uzito wa juu na bingwa wa dunia, Lennox Lewis amemwambia mwanamasumbwi, Anthony Joshua kuwa aachane na mwalimu wake ambaye anamfundisha, Rob McCracken kutokana na mchezaji huyo kupokea kichapo kutoka kwa Andy Ruiz.
Lennox Lewis amemwambia, Anthony Joshua kumuachisha kazi kocha wake Rob McCracken baada ya kipigo Andy Ruiz
McCracken amekuwa kocha wa Anthony Joshua kwa muda mrefu sasa huku akimpatia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Olympic gold, IBF, WBA na WBO lakini Lewis anaamini anapaswa mwalimu huyo kuachananaye hasa kutokana na matokeo hayo ya haibu aliyopata kwenye ukumbi wa Madison Square Garden siku ya Jumamosi.
Tokeo la picha la Andy Ruiz
”Ninasema huwezi kwenda ulimwenguni huku ukiwa na mwalimu wa daraja la tatu, hawezi kuwa na jibu la maswali yako kwa levo yako unayotaka, unahitaji kuwa na ‘professor’.
”McCracken ni A1 pasipo hata kuuliza, lakini pengine hafiti kwa mfumo wa AJ ambao anahitaji kupambana. McCracken pengine sio mtu sahihi kwa mfumo wa upiganaji wa AJ, hata upande wao ulionekana haukujiandaa kwaajili ya hili pambano lao”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment