Wednesday, June 19, 2019
Aibu 20 za Wanaume Endapo Mwanaume Atafanya Haya Kwenye Mahusiano ya Mapenzi
AIBU 20 ZA WANAUME:
1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume kulishwa na mkewe.🙈
2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo ukakala ukakoroma na taulo ukafunga..🙈
3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.🙈
4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako wanajua kuwa anakuzidi uwezo.🙈
5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia urefu wa kimo🙈
6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo na watoto wote kisa yeye anazohela🙈
7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa🙈
8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti kutoka kwake.🙈
9. Ni aibu na fedheha kupewa zawadi ya kiwanja na wakwe zako siku ya send off.🙈
10. Ni aibu na fedheha kujenga kwenye kiwanja cha mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki kiwanja🙈
11. Ni aibu na fedheha kulelewa mtoto wako na baba wa kambo wakati wewe upo unaishi na unajiita kidume🙈
12. Ni aibu na fedheha kukaa kwenye nyumba yenye fenicha zoote kanunua mkeo🙈
13. Ni aibu na fedheha kusimamia ujenzi wa nyumba ya mkeo wakati wewe huchangii hata shilingi mia🙈
14. Ni aibu na fedheha kulea mtoto ambaye sio wa kwako kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu wakati mkeo anajua mtoto yule sio wa kwako.🙈
15. Ni aibu na fedheha kulala kimapenzi na mwanamke ambaye anajua kuwa wewe unajua na unaushahidi wa michepuko yake🙈
16. Ni aibu na fedheha kumbembeleza mwanamke anayejua kuwa anakukosea kwa makusudi🙈
17. Ni aibu na fedheha kumaliza makanisa ukiwahadithia wachungaji tabia mbaya na usaliti wa mkeo🙈
18. Ni aibu na fedheha mkeo kukunyima unyumba ukaenda kumshitaki kwa wazazi wake wakati unajua cha kufanya🙈
19. Ni aibu na fedheha mara kukopakopa kwa wakwe zako tena waliostaafu kazi..ni aibu ni aibu kubwa.🙈
20. Ni aibuu na fedheha kwenda baa na mke baa au sehemu za starehe kila siku ikija bili unapewa wewe nawe unampa mkeo alipe kazi kukuna tu kidevu na kwenye wallet umejaza business card na viwembe vya kugushi nyaraka mitaani🙈
Hizo ni baadhi tu ya aibu za wanaume waliowengi karne ya leo. Sambaza kwenye ma group wajijue na wamuombe Mungu awafungulie milango nao wawe wanaume katika nyumba zao🙈🙈🙈🙈🙈
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment