Friday, May 24, 2019

Kwa Mara ya Kwanza Nikk wa Pili Aonyesha Sura ya Mtoto wake



Kwa mara ya kwanza mwimbaji kutokea kwenye game ya Hip Hop kutokea kwenye kampuni ya WEUSI Nikk Wa Pili ameonyesha sura ya mtoto wake wa kike Zuri kupitia ukurasa wake wa instagram leo May 23,2019.

Nikk Wa Pili ambaye tayari ameshamchumbia mpenzi wake Joan miezi kadhaa iliyopita walibahatika kumpata mtoto huyo siku ya April 23,2019 hii ni kwa mujibu wa kile ambacho Nikk alikiandika kupitia mtandao wa WhatsApp. Nikk Wa Pili anakua miongoni mwa mastaa ambao wamebarikiwa kupata mtoto kwa mwaka huu wa 2019.

” Habari! dunia semeni hi kwa mtoto wangu zuri” aliandika Nikk Wa Pili kupitia kupitia ukurasa wake wa instagram.

No comments:

Post a Comment