Bongo fleva ndio sehemu ambayo mashabiki wanapenda wasanii wao kuliko muziki wenyewe wanaoufanya? Yaani wapo radhi kusupport kitu chochote hata ikiwa siyo ilimradi tu ni cha msanii wao kipenzi na wapo radhi kupinga cha msanii mwingine hata kama ni kizuri?
Hiki ndo kiwanda ambacho sifa za kuwa meneja ni zaidi ya kuwa na kipawa na uwezo wa kuongoza msanii. Hapa sifa kubwa ni kujua kucheza michezo michafu na uwezo wa kuinfluence media icheze nyimbo za msanii fulani hata kama uwezo ni mdogo
Hiki ndo kiwanda wasanii hawapendi kujifunza kwa wenzao na wao huamini siku zote wenzao wapo sehemu walipo kw kuwa tu wanabebwa na wala sio kwakuwa uwezo wao una waruhusu kua pale walipo. Bongo fleva ni sawa na mwanamke mzuri mwenye kila sifa ya sura,umbo na muonekano ila mwenye tabia chafu na zenye kuudhi kiasi akiacha hizo tabia chafu atakuwa ni moja kati ya wanawake bora kuwahi kutokea.
No comments:
Post a Comment