Thursday, May 30, 2019
Chelsea Yatwaa Kombe la Europa League kwa Kuichapa Arsenal
Ilihitajika ushindi tu kwa Chelsea kuweza kupata tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao na kuwa mabingwa wa kombe la Europa baada ya kuichapa Arsenal kwa mabao 4-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa jana.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Oliver Giroud dakika ya 17, Pedro dakika ya 60, Eden Hazard aliyefunga mawili dakika ya 65 kwa penati na dakika ya 72 huku Arsenal wakipata la kufutia machozi kupitia kwa Iwobi.
Licha ya kupata changamoto ya kukosekana kwa mashabiki wake katika mchezo wa fainali hiyo kutokana na timu hizo kutoka umbali mrefu, huku uwanja ukiwa na mashabiki 5,000 kutoka pande zote mbili ulioonekana kujaa nusu nchini Azerbaijan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment