Friday, May 31, 2019
Kisa cha Ferooz, Luludiva Kuwasaidia Wahudumu wa Baa
Msanii wa muziki wa bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Luludiva anaetamba na wimbo wa mapopo amesema kwa sasa ameandaa mpango maalumu kwaajili ya mabinti wanaofanya shughuli za uhudumu wa baa
Kwenye mahojiano na dozenselection Luludiva amesema kuwa ameamua kuja na mpango wa kuanzisha Foundation kwaajili ya kuwasaidia wahudumu wa baa hasa mabinti wanaonyanyasika na kudharaulika.
Ameongeza kuwa hata yeye alipitia huko kwani aliwahi kuwa mhudumu wa baa kabla ya kuwa staa wa muziki hivyo anatambua manyayaso, dharau na matusi wanayokumbana nayo wahudumu hao.
Ameongeza kuwa lengo kubwa la kuanzisha foundation hiyo ni kuwapa ushawishi na kuwasaidia pale itakapo wezekana ili waweze kutimiza malengo yao.
Balozi huyo wa Kampuni ya simu ya infinix ameongeza kuwa hakuwahi kulipwa alipokuwa anafanya kazi ya uhudumu wa baa kwa mkongwe wa muziki Ferooz na kwamba alifanya kazi hiyo kwa kudharaulika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment