Wednesday, May 1, 2019

Kiki aliyokuja nayo SoujalBoy yamtokea puani, akutana na rungu la kutumikia jela kwa siku 240 kwa kosa hili

Rapper kutoka Marekani DeAndre Cortez Way alimaarufu Soulja boy ambaye wengi walidai amerudi kwenye game kwa kupitia kiki ya kuwadis wasanii wenzake kama akina Tyga, Drake na Kanye West imemtokea Puani.



Baada ya rapper huyo Kukaa Ndani ya Jela Kwa miezi 8 ambayo ni sawa na Siku 240 Jela kwa kosa la kuvunja na kukiuka masharti ya muda wa uangalizi ambayo yaliwekwa na mahakama yaani Probation

Siku chache zilizopita Rapper SouljaBoy Alikutwa Akimiliki Silaha Nyumbani kwake Kitu ambacho ni kinyume na makubaliano ya kesi yake ya kumiliki silaha ya Mwaka 2014.

SouljaBoy alishindwa kumshawishi Jaji ambae alikuwa Akiendesha Kesi yake Jumanne Hii na Akashindwa Kutoa Vigezo ambavyo vingefanya apungiziwe adhabu ya kifungo hicho ambacho kimeanza leo .



.
Rapper huyo Ameandikiwa Pia Adhabu nyingine ambayo siku akitoka tu Jela Atatakiwa Kutumikia Siku Nyingine 40 kwa Kushiriki Kazi Tofauti za Jamii ambazo atapangiwa Kwa Kipindi Hiko.

By Ally Juma.

No comments:

Post a Comment