Taifa Stars yasonga mbele hatua ya kufuzu michuano ya CHAN
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars imefanikiwa kusonga mbele kwenye hatua za kufuzu kushiriki michuano ya CHAN kwa kuifunga Kenya goli 1-4 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Hatua ya mikwaju ya penati imekuja baada ya timu hizo kutoka sare 0-0 ndani ya Dakika 90 za kawaida.
Kwa matokeo hayo Tanzania inasonga mbele na Kenya wameshatolewa kwenye hatua ya kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya CHAN.
No comments:
Post a Comment