Thursday, July 25, 2019

Picha iliyomfanya Rihanna atake kuangusha simu yavunja rekodi



Stori kubwa iliyotrend kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na picha ya binti mdogo ambayo ameipost mwimbaji Rihanna kupitia ukurasa wake wa instagram na wengi kudhani kuwa huenda mtoto yule ni Rihanna alivyokuwa mdogo.

Picha hiyo imeonekana kusambaa kwa kasi kubwa siku ya leo July 24,2019 huku Rihanna akiwa ameandika caption iliyosomeka “Nusu niangushe simu yangu, kivipi?” , komenti zimekuwa nyingi na kila mtu ameandika wazo lake kuhusiana na picha hiyo ambapo wengine kuhisi kuwa huenda Rihanna akawa na undugu na mtoto huyo kutokana na wawili hao kufanana.

Mpaka sasa picha hiyo ina jumla ya likes milioni 6.3 na comments elfu 79 ndani ya saa 15 tokea ipostiwe  kwenye ukurasa halali wa mwimbaji huyo na kutajwa kuwa ni miongoni mwa picha ambazo zimeingia kwenye rekodi ya kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi.

Mwaka 2017 Beyonce alivunja rekodi ya kupata likes Milioni 6.3 ndani ya saa 8 baada ya kupost picha aliyotangaza juu ya ujauzito wake wa watoto mapacha na kumpiku Selena Gomez ambaye alishikilia  rekodi ya likes Milioni 6.3 kwenye picha aliyoipost June 25 2016.

No comments:

Post a Comment