Wednesday, July 3, 2019

Mrembo Tunda Afunguka "Mimba Nimesingiziwa Sana Kama Kweli Ningekuwa na Watoto Watano Sasa'

Tunda Kama Mimba Nishabambikiwa Sana

Muuza nyago maarufu kwenye video za Kibongo, Tunda amefunguka kuwa kama kubambikiwa mimba anaongoza kwani angekuwa na watoto zaidi ya watano.

Akipiga stori na Za Motomoto, Tunda alisema kuwa anachukizwa na watu wanaoibuka na kudai kuwa Tunda ana ujauzito huku yeye mwenyewe akiwa hajui chochote kinachoendelea kiasi ambacho vitu vingine anaamua kunyamaza tu.

“Kama ni mimba tu za kuzaa kwa maneno ya watu basi ningekuwa na watoto zaidi ya watano maana kila kukicha Tunda ana mimba sijui nini vitu kibao ambavyo hata mimi mwenyewe muhusika sivijui kabisa kabisa,” alisema Tunda.

No comments:

Post a Comment