Tuesday, July 2, 2019
Je, Mo Dewji kuileta Arsenal nchini ? ‘Tunataraji kuwa nanyi Tanzania hivi karibuni, asante kwa jezi iliyosainiwa’
Katika maelezo ya Dewji kupitia akaunti yake ya Instagram, ameandika ujumbe wa kuishukuru klabu hiyo kwa zawadi hiyo huku akisema kuwa anatarajia kuwa nao hapa nchini hivi karibuni swala ambalo linawaacha mashabiki wa soka kwenye maswili kuwa je vijana hao wa The Gunnersa wanatarajia kutua Tanzania ?.
“Asante @Arsenal kwa jezi iliyosainiwa! Natarajia kutafuta njia za ushirikiano na @SimbaSCTanzania. Tunataraji kuwa nanyi Tanzania hivi karibuni. πΊππππππ ππ π¨ππππππ π ππππ ππ πππππππ ππ π¨ππππππ!,” – ameandika Mo Dewji.
//
Mohammed Dewj ameongeza “Thank you @Arsenal for the signed kit! I look forward to exploring avenues for partnership with @SimbaSCTanzania. We look forward to having you in Tanzania soon. Karibu πΉπΏ
πΆπππ π ππππππ ππππππ π ππππππ!”
Kila ifikapo tarehe 08/08 ya kila mwaka timu ya Simba hufanya bonanza linalojulikana kama Simba Day ambapo hucheza na timu alikwa kutoka katika nchi nyingine huku ikitumia nafasi hiyo kama sehemu ya kuwatambulisha wachezaji wao wapya. Arsenal itakuja nchini kucheza na miamba hiyo ya soka ya Tanzania siku ya Simba Day ?, tusubiri tuone.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment