Mastaa kutoka Nigeria, Davido na Wizkid wamethibitisha ujio wa kazi yao mpya kupitia kurasa zao rasmi za mtandao wa Instagram.
Ujumbe alioanza kupost Davido kwenye Insta story yake ulisomeka hivi, ”My brother Wizkid make we finish dem”. Wizkid nae alichukua ile post ya Davido na kuipost kwake huku akiandika 'One time my G'.
Kupitia jumbe hizo za kwenye Insta story zao, zinaonyesha kuna Project inaendelea kati ya hawa watu wawili licha ya hapo nyuma kusemekana wana bifu ingawa walilimaliza kwa kualikana kwenye sho zao.
No comments:
Post a Comment