Thursday, April 25, 2019
Panga Kali Man United Kurejesha Makali ya Timu
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer inasemekana anajipanga kufyeka mastaa kadhaa ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kusuka upya kikosi chake, Solskjaer anataka kutengeneza timu ambayo itarejesha makali ya timu hiyo kama ilivyokuwa enzi za zamani za kocha Alex Ferguson.
Nyota wanne ndio wanatajwa kuwa ndio wamekalia kuti kavu katika mipango hiyo ya Solskjaer ya kutembeza panga. Mastaa hao ambao wanalaumiwa kwa kushuka kiwango katika siku za LONDON, England Panga kali Man United karibuni ni pamoja na Chris Smalling, Ashley Young, Nemanja Matic na Romelu Lukaku.
Solskjaer inasemekana amechukizwa na kitendo cha mastaa hao kuporomoka kiwango. Kocha huyo aliteuliwa kufundisha kwa muda timu hiyo, Desemba mwaka jana ambapo alipata matokeo mazuri mwanzoni na wachezaji kuonekana kujituma. Hata hivyo, upepo uligeuka ghafl a baada ya kupewa mkataba wa kudumu, Machi 28, mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment